Jumapili 22 Februari 2026 - 11:40
Nafasi ya Siri ya Israel Katika kuvishambuli vitu vitakatifu vya Mashia Nchini India

Hawza/ Syed Kalbe Jawad Naqvi, Katibu Mkuu wa Majlis Ulama-e-Hind, katika hotuba yake huku alizungumzia tukio la kuvunjiwa heshima Husseiniya moja wakati wa operesheni ya vikosi vya polisi mjini Bhopal, pamoja na shambulizi na uchomaji moto wa raudha inayonasibishwa na Amirul-Mu’minin Ali (as) katika mji wa Farrukhabad, jimbo la Uttar Pradesh nchini India. Aliyataja matukio hayo kuwa ya kutia shaka na yaliyopangwa kwa utaratibu, akisisitiza kuwa, kuna mkono wa wahusika wanaohusishwa na Israel wenye lengo la kudhoofisha mshikamano na umoja wa kidini nchini India.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza,  Syed Kalbe Jawad Naqvi alieleza kuwa; kudhalilishwa kwa Husseiniya wakati wa hatua ya polisi mjini Bhopal na pia shambulizi pamoja na uchomaji moto katika raudha inayohusishwa na Imam Ali (as) katika mji wa Farrukhabad, jimbo la Uttar Pradesh, ni matukio yenye dalili za upangaji maalumu. Alisisitiza kwamba; wahusika wanaodaiwa kuwa na uhusiano na Israel wanahusika katika matukio hayo kwa lengo la kuvuruga hali ya kuishi kwa pamoja na umoja wa kidini nchini humo.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, aligusia historia ya mahusiano ya kidini nchini India akisema kuwa; ingawa kumewahi kutokea migogoro ya kimadhehebu kati ya Wahindu na Waislamu katika historia ya nchi hiyo, lakini haijawahi kutokea kwa Mashia kulengwa kwa njia ya kupangwa na kuratibiwa. Alisema hali inayoonekana sasa katika baadhi ya maeneo ni ishara ya mwelekeo hatari unaohitaji radi amali ya haraka kutoka kwa serikali za majimbo, hasa Madhya Pradesh na Uttar Pradesh.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wanazuoni wa India, aliitaka serikali kuu ya India kuyachunguza kwa umakini matukio hayo, kuunda kamati maalumu ya uchunguzi, na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika—waliotekeleza na waliotoa amri—ili kuzuia kurudiwa kwa matukio kama hayo. Alionya kuwa, kupuuzia matukio haya kunaweza kufungua mlango wa kuenea kwa ukosefu wa usalama na kuchochea hisia za kidini katika jamii.

Mwanazuoni huyo mashuhuri wa India, pia alieleza uwezekano wa kuwepo kwa “wahusika wanaohusishwa na Israel” katika kuanzisha mvutano huo. Alidai kuwa; hatua hizo huenda zikawa na lengo la kuvuruga mazingira ya kuishi kwa pamoja kidini nchini India, na kwamba misimamo ya Mashia inayopinga sera za Marekani na Israel katika uwanja wa kimataifa huenda ikawa sababu ya kuchochea harakati kama hizo.

Mwisho, alisisitiza kuwa; serikali inapaswa kufanya uchunguzi wa wazi na wa kina ili kubainisha ukweli, na kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wa vitendo hivyo vya uchochezi, ili kulinda usalama na kuendeleza kuishi kwa amani katika jamii ya India.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha